Viongozi wa dini watakasa nyumba ya mbunge wa Molo

Tom Mathinji
1 Min Read
Mbunge wa Molo Kuria Kimani.

Viongozi kadhaa wa kanisa jana Ijumaa, walikusanyika nyumbani kwa mbunge wa Molo, Kuria Kimani, kwa shughuli ya utakasaji kufuatia uharibifu uliotekelezwa nyumbani kwake siku ya Jumanne wakati wa maandamano dhidi ya mswada wa fedha.

Maandamano hayo yaliyochochewa na ghadhabu zilizotokana na kupitishwa kwa mswada huo unaopendekezwa ambapo mamia ya vijana waliandamana barabarani katika sehemu mbalimbali nchini kuupinga.

Mjini Molo, maandamano hayo yalisababisha uharibifu mkubwa nyumbani kwa mbunge Kimani.

Waandamanaji waliokuwa na hasira walivuka ukuta uliozingira nyumba yake na wakateketeza na kuharibu magari na kupora mali. Baadhi ya wale waliovamia makazi yake waliiba mifugo pia.

Maombi na nyimbo za injili zilisimbwa kwenye sherehe hiyo iliyoandaliwa kwenye uwanja wa makazi ya Kimani.

Mbunge huyo ni mwenyekiti wa kamati ya bunge la taifa kuhusu fedha iliyoshughulikia mswada huo.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *