Muungano wa makanisa na viongozi wa dini nchini CCAK, umelalamikia uamuzi wa serikali wa kukomesha usajili wa makanisa na mashirika zaidi ya kidini nchini.
Mwenyekiti wa muungano huo kasisi Hudson Ndeda ambaye alikuwa akizungumza huko Meru, alisema kwamba agizo la kukomesha usajili huo liliondolewa mwezi Juni mwaka jana na walitarajia kwamba serikali ingeaza kusajili makanisa.
Kasisi Ndeda anasema kwamba maombi ambayo wachungaji wamekuwa wakiweka kwa afisi mwanasheria mkuu ya kusajili makanisa mapya tangu juni mwaka jana hayajajibiwa hata baada ya agizo la kusitisha usajili huo kuondolewa.
Mungano huo sasa unaitaka afisi ya mwanasheria mkuu ishughulikie maombi ya usajili wa makanisa mapya ambayo wanasema yamezidi elfu moja kufikia sasa.
Viongozi hao wa dini wanataka kufahamishwa na afisi hiyo ya mwanasheria mkuu iwapo kuna tatizo katika usajili wa makanisa mapya nchini ili watoe usaidizi kulingana na uwezo wao.
Usajili wa makanisa na mashirika ya kidini ulisitishwa mwaka 2014 kufuatia ripoti kwamba mashirika ya kidini na makanisa yalikuwa yakitumiwa kutoa mafunzo ya itikadi kali.
Agizo hilo liliondolewa mwezi juni mwaka jana lakini masharti mapya ya usajili yakawekwa likiwemo hitaji la kiongozi wa dini kuwa na shahada au stashahada katika masomo ya dini.
Ripoti yake Jeff Mwangi.