Watu 15 kusailiwa kwa wadhifa wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

Marion Bosire
1 Min Read

Jopo la kuchagua watu watakaosailiwa kwa wadhifa wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma lilitoa taarifa Jumamosi kusema kwamba limeteua watu 15 kati ya wote waliotuma maombi.

Waliopo kwenye orodha hiyo ni Thomas Letangule, Taib ali Taib, Danstan Omari, Jacinta Nyaboke, Victor Mule, Tabitha Ouya na David Kiplagat Ruto.

Wengine ni Francis Andayi Weche, Winston Ngaira,Peter Mungathia Mailanyi anayewakilisha walemavu, Lilian Akinyi, Jacob Nyakundi, James Wahome Ndegwa, David Mogunde Okachi na Renson Mulele Ingonga.

Tume ya utendakazi wa umma yaani Public Service Commission – PSC itatekeleza usaili wa watu hao Agosti 2 na 3 mwaka huu wa 2023.

Wadhifa huo ulisalia wazi baada ya aliyekuwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji kuteuliwa na rais William Ruto kuongoza huduma ya kitaifa ya ujasusi yaani National Intelligence Service – NIS.

Wakenya wamepatiwa fursa ya kutoa habari za kuaminika kuhusu ufaafu au kutofaa kwa yeyote aliye kwenye orodha hiyo kuteuliwa kwa wadhifa wa mkurugenzi wa mashtaka ya umma. Taarifa hizo zitakuwa za kiapo.

Tangazo hilo lilikuwa limetiwa saini na mkurugenzi mtendaji wa tume ya utendakazi wa serikali Shadrack Mose, ambaye pia ni mwenyekiti wa jopo la kuteua wa kusailiwa kwa wadhifa huo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *