Vijana na kina mama wahimizwa kusajili kampuni Kwale

Marion Bosire
1 Min Read

Gavana wa Kaunti ya Kwale Fatuma Achani ameendeleza kampeni ya kushawishi vijana na kina mama katika kaunti hiyo kusajili makundi yao kuwa kampuni ili waweze kufanya biashara na serikali na sekta ya kibinafsi katika kaunti hiyo.

Achani alikuwa ameandamana na naibu wake Chirema Kombo kwa uzinduzi wa makundi ya Sambamba Malungoni women Group, Kampuni ya kina mama ya Kudzecha pamoja na kampuni ya vijana ya Wanne Legends yaliojisajili kuwa kampuni huko wadi Puma katika eneo bunge la kinango.

Amesema kuwa serikali yake inalenga kuinua viwango vya kiuchumi kwa akina mama na vijana kwale kupitia utoaji wa zabuni kwa makundi yaliyojisajili kuwa kampuni

Kufikia sasa kampuni 12 za akina mama katika kaunti hiyo zimpata zabuni huku Damwa women limited kutoka wadi ya Samburu-Chengoni huko Kinango ikiwa ni kampuni ya hivi punde ya akina mama iliyopata zabuni.

Inahusu ujenzi wa barabara ya Chiphangani ya kilomita 8 itakayogharimu shilingi 4. Mkurugenzi wa kampuni hiyo Joyce Mgunya amedokeza kuwa hatua hiyo itawakuza kiuchumi.

Share This Article