Mahakama ya rufani imefutilia mbali kifungo cha miaka 67 gerezani alichohukumiwa mbunge wa Sirisia John Waluke na mshirika wake wa zamani wa kibiashara Grace Wakhungu.
Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kujipatia shilingi milioni 313 kwa njia ya ulaghai kutoka kwa shirika moja la serikali.
Walikuwa wamehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 60 gerezani kila mmoja au faini mbadala ya zaidi ya shilingi bilioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kupokea pesa hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa hamashauri ya kitaifa ya mazao na nafaka, (NCPB) kwa mahind ambayo hayakuwasilishwa.
Mahakama hiyo iliarifiwa kwamba kulikuwa na kasoro zilizotatiza kesi ya upande wa mashtaka na kudumisha kwamba shughuli hiyo ilikuwa ya kibiashara na madai hayo hayakuwa ya kiuhalifu na hivyo hawakuwa wametenda uhalifu.
Kwenye uamuzi wao majaji Asike Makhandia na Patrick Kiage walisema wameridhika kwamba waliowasilisha rufaa walithibitisha kesi yao na hivyo mahakama ikaidhinisha rufaa hiyo.
Justice Abida-Ali Aroni hata hivyo alikataa kutia saini hukumu hiyo.