Vidosho wa Kenya kufungua Kombe la Dunia dhidi ya Uingereza

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa akina dada walio chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Junior  Starlets,  imejumuishwa kundi C pamoja na Uingereza kwenye fainali za  Kombe la Dunia katika Jamhuri ya Dominika.

Mataifa mengine kundini humo ni Korea Kaskazini na Mexico.

Junior Starlets watafungua kampeini  dhidi ya Uingereza Oktoba 17, kabla ya kuikabili Korea Kaskazini siku tatu baadaye, na kuhitimisha ratiba dhidi ya Mexico Oktoba 23.

Kenya itashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza katika histori.

Nigeria wamo kundi A pamoja New Zealand, Ecuador na wenyeji Dominican.

Uhispania,Marekani, Korea Kusini na Colombia wanaunda kundi  B, huku lile la D likisheheni Brazil,Zambia,Poland na Japan.

Kipute hicho kitaandaliwa kati ya Oktoba 16 na November 3 mwaka huu.

Website |  + posts
Share This Article