Gavana Ndeti alalamikia ucheleweshaji wa fedha kwa kaunti

Martin Mwanje
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti ametoa wito kwa Wizara ya Fedha kutoa fedha kwa kaunti kwa wakati unaofaa ili kuziwezesha serikali za kaunti kutoa huduma bora kwa raia. 

Gavana Ndeti amesema kaunti zinaendelea kukumbana na wakati mgumu katika utoaji wa huduma kwa raia kutokana na ukawishaji wa fedha hizo.

Ameongeza kuwa kaunti yake ilipokea mgao wa fedha wa mwezi Novemba kutoka kwa Wizara ya Fedha wiki iliyopita.

Licha ya fedha hizo kukawia kutolewa, Ndeti anasema serikali yake imeendelea kulipa mishahara na kutoa huduma bila kufeli kutokana na matumizi bora ya fedha.

Aliyasema hayo katika eneo la Ekalakala huko Masinga wakati wa makongamano ya ushiriki wa raia kwenye mkakati wa fedha wa kaunti hiyo wa mwaka 2024.

Magavana wamekuwa wakiinyoshea serikali kuu kidole cha lawama kwa kuchelewa kutoa mgao wa fedha kwa serikali za kaunti katika hatua wanayosema imeathiri utoaji huduma kwa raia.

 

Share This Article