Mzozo unatokota kuhusu ujenzi wa soko jipya la kisasa eneo la Makindu kaunti ya Makueni kati ya viongozi wa maeneo ya Kibwezi na Gavana Mutula Kilonzo Jnr huku mbunge wa Kibwezi West Mwengi Mutuse, akitishia kuongoza maandamano iwapo soko hilo litaamishiwa kwingine.
Sio mara ya kwanza wanasiasa kuonekana kuvutana kuhusiana na ubabe wa ujenzi wa masoko mapya na serikali kuu na ile ya kaunti baada ya mzozo saweia kushuhudiwa mjini Thika.
Wakati huo uo mbunge huyo amemsuta gavana Mutula Kilonzo Junior kwa kile amesema ni kutengwa ki-maendeleo kwa maeneo bunge yote ya Kibwezi akitaka ugavi sawa wa rasilimali kutoka kwa serikali ya kaunti.
“Hakuna kiongozi ukue Gavana ukue Seneta atapinga maendeleo Kibwezi kama unataka kupinga maendeleo utafute kwingine, Tumeamua tutajenga soko Makindu na hizo barua unaandika ati soko ihamishwe kutoka Makindu kwenda Wote hiyo haitawezekana.”akasema Mutuse
Mbunge huyo pia amelalama kuhusu kubaguliwa kwa wakaazi wa Kibwezi katika nyadhfa za uongozi katika serikali ya kaunti ya ya Makueni.
“Kama haitafanya I will mobilise my people tukatae kulipa kodi.”akaongeza Mutuse