Utapiamlo waripotiwa Gaza

Marion Bosire
2 Min Read

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Palestina huko Gaza limesema kwamba utapiamlo unaenea kwa kasi kati ya watoto wa eneo hilo.

Hata yanajiri wakati ambapo Israel iko tayari kutuma ujumbe wake nchini Qatar kwa mazungumzo mapya ya kutafuta kusitisha mapigano Gaza.

Jumamosi shirika hilo la UNRWA lilisema kwamba mmoja kati ya watoto watatu walio chini ya umri wa miaka miwili huko Gaza Kaskazini ameathiriwa na utapiamlo.

Taarifa hiyo ilitolewa kupitia akaunti za mitandao ya kijamii za UNRWA.

Ijumaa Israel ilitangaza kwamba itatuma wawakilishi wake Qatar kwa ajili ya mazungumzo baada ya kundinla Hamas kutoa pendekezo jipya la kusitisha mapigano na kubadilishana mateka na wafungwa.

Taarifa zinaashiria kwamba ujumbe wa Israel utaongozwa na mkuu wa shirika la kijasusi la Israel Mossad David Barnea.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anapanga mkutano wa usalama wa baraza la mawaziri kabla ya mazungumzo hayo kuanza.

Afisi ya waziri huyo mkuu inasemankwba masharti ya Hamas kwenye pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza sio ya kweli.

Juhudi za kuafikia mapatano ya kusitisha mapigano Gaza kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan hazikuzaa matunda huku Israel ikipanga kushambulia eneo la Rafah Kusini mwa Gaza.

Chasela wa Ujerumani Olaf Scholz, ambaye anazuru eneo hilo kwa siku mbili alilalamikia shambulizi linalopangwa la Rafah eneo ambalo zaidi ya nusu ya wakazi wa Gaza wamekimbilia.

Share This Article