Utalii: Wakenya kuzuru mbuga za kitaifa bila malipo Septemba 28

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakenya watapata fursa adimu ya kuzuru mbuga za kitaifa kote nchini Septemba 28 mwaka huu. 

Hii itakuwa siku moja baada ya Kenya kuungana na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Utalii Duniani.

Waziri wa Utalii Rebecca Miano anasema hatua hiyo iliidhinishwa jana Jumanne wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi.

Lengo ni kupigia debe utalii wa humu nchini.

Wakenya wanajulikana kutokuwa na utamaduni wa kutembelea mbuga za kitaifa na maeneo mengine ya kitalii nchini, yamkini kutokana na gharama na sababu nyinginezo.

Kutokana na tangazo hilo, miongoni mwa mbuga ambazo Wakenya wanatarajiwa kuingia bila malipo ni mbuga ya kitaifa ya Tsavo, Amboseli, Maasai Mara na mbuga ya kitaifa ya Nairobi miongoni mwa zingine.

Share This Article