Mabingwa wa kombe la shirikisho la soka barani Afrika klabu ya USM Algers kutoka Algeria ndio mabingwa wapya wa kombe la CAF Super kwa mara ya kwanza baada ya kuwalaza mabingwa wa kombe la ligi ya mabingwa Al Ahly kutoka misri bao moja kwa bila .
Nahodha Zinedine Belaid alitikisa nyavu kwa golo la pekee na la ushindi kupitia kwa penati ya kipindi cha kwanza kwenye fainali iliyosakatwa Ijumaa usiku nchini Saudi Arabia.
Ahly maarufu kama Red Deveils walikuwa wakisaka kombe la Super kwa mara ya 9 lakini bahati ina miujiza kweli na ilikuwa upande wa vijana kutoka Algiers.