Serikali inapanga kuongeza ushuru thamani wa ziada, VAT unaotozwa kwa bidhaa kutoka asilimia 16 hadi 18.
Lengo la kupandisha ushuru huo ni kuianisha na asilimia 18 ya ushuru wa VAT unaotozwa na mataifa mengine jirani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.
Hili likitekelezwa litaongeza bei ya bidhaa zote zinazotozwa ushuru wa VAT na kufanya gharama ya maisha kupanda zaidi.