Serikali ya kaunti ya Nakuru imezindua zoezi la usambazaji wa mbolea ya bei nafuu kwa ghala zilizoidhinishwa katika kaunti hiyo kabla ya kuanza kwa msimu wa upanzi.
Mbolea hiyo kisha itatolewa kwa wakulima katika hatua inayolenga kupiga jeki uzalishaji wa chakula katika kaunti hiyo.
Leo Jumatatu, mbolea hiyo iliwasilishwa katika ukumbi wa jamii wa Keringet na ghala ya bodi ya nafaka ya Kiptororo katika kaunti ndogo za KN na KS.
“Hii ni kuendana na dhamira yangu ya kuhakikisha awamu ya mwisho ya usambazaji wa mbolea ya bei nafuu kwa ghala zilizoidhinishwa katika kaunti unafanyika kabla ya kuanza kwa msimu wa upanzi,” alisema Gavana Susan Kihika katika taarifa.