Usalama wazorota eneo la Shikhambi, Kakamega

Martin Mwanje
1 Min Read
Maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Central mjini Kakamega wanawazuilia washukiwa wawili kwa tuhuma za kuwahangaisha wakazi na kushiriki visa vya uhalifu.
Hii ni baada ya washukiw ahao kupatikana na bidhaa za wizi huku kamera za usalama, CCTV zikionyesha wengine, akiwemo mwanafunzi wa darasa la nane wakiwa katika shule moja eneo bunge la Lurambi.
Kamera hizo ziliwanasa washukiwa wakibomoa milango na kuiba bidhaa za wakazi eneo la Shikhambi viungani mwa mji wa Kakamega.
Kulingana na wakazi, visa vya wizi vimekithiri huku wakiwalaumu maafisa wa polisi pamoja na mahakama kwa kuwaachilia washukiwa ambao wamepatikana na mali za wizi.
Wakazi hao wametishia  kujichukulia sheria mikononi.
Maafisa wa nyumba kumi eneo hilo, wakiongozwa na Ruben Otiende na Alfred Amambia, wanasema wanapitia hali ngumu ya kupambana na wezi hao, ambao pia wanawatishia mara tu wanapoachiliwa.
Share This Article