Usaili wa Mwenyekiti na Makamishna wa IEBC wakamilika

Jopokazi hilo litawasilisha majina ya waaniaji wawili bora kwa Rais  Ruto, ambaye atawasilisha jina moja kwa bunge la kitaifa ili kuidhinishwa.

Dismas Otuke
2 Min Read
Chairperson IEBC selection panel Dr Nelson Makanda with Vice Chair person Ms Charity Kisotu consult after addressing the press on March.6th.2023/EZEKIEL AMING'A

Mchakato wa usaili wa mwenyekiti na makamishna wa tume huru ya  uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini (IEBC), umekamilika rasmi leo baada ya kudumu kwa mwezi mmoja .

Jopo hilo litaanza likizo tarehe 28 mwezi huu ili kuandaa ripoti na majina ya orodha ya mwisho inayotarajiwa kuwasilishwa kwa Rais William Ruto, kufikia tarehe 9 mwezi ujao.

Jopokazi la usaili likiongozwa na mwenyekiti Nelson Makanda, lilikalimisha kuwahoji waaniji wa kiti cha mwenyekiti tarehe 26 mwezi uliopita, ambapo jumla ya watu 11 walihojiwa, wakiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya utekelezaji katiba Charles Nyachae, na aliyekuwa msajili wa idara ya mahakama Anne Amadi.

Wengine waliosailiwa kwa mwenyekiti wa IEBC ni Saul Simiyu Wasilwa, Abdulqadir Lorot Ramadhan, Joy Mdivo, Edward Katama Ngeywa, Erastus Edung Ethekon, Francis Kakai Kissinger, Jacob Ngwele Muvengei, Lilian Wanjiku Manegene, na Robert Akumu Asembo.

Jopokazi hilo litawasilisha majina ya waaniaji wawili bora kwa Rais  Ruto, ambaye atawasilisha jina moja kwa bunge la kitaifa ili kuidhinishwa.

Usaili wa makimishna ulishirikisha watu 111 walioalikwa huku 106, wakihudhuria na wengine watano wakikosa kujitokeza.

Kulingana na sheria, jopokazi hilo litawasilisha majina ya watu tisa bora kwa nafasi hizo za makamishna kwa Rais Ruto, ambaye atawasilisha majina sita kwa bunge ili kuidhinishwa.

 

Website |  + posts
Share This Article