Mahakama moja ya kijeshi nchini Uganda, siku ya Jumatatu ilimhukumu mwanamume wa miaka 43 kifugo cha miaka 41 gerezani, kwa mauaji ya kiongozi wa kidini.
Mahakama hiyo ya kijeshi yenye makao yake eneo la Makindye, ikiongozwa na brigedia Jenerali Freeman Mugabe, ilitoa hukumu hiyo kwa Biasaali Mugoya baada ya kukiri kumuua Sheikh Masuud Mutumba, katika wilaya ya Bugiri.
“Baada ya kusikiza pande zote mbili, mahakama imeamua kwamba hukumu ya kosa hilo ni kifo. Mugoya ana jamii, na amekuwa korokoroni Kwa muda wa miaka mitatu…hukumu ya miaka 45 gerezani ni sahizi,” Jenerali Mugabe aliamua.
Hata hivyo baada ya kuzingatia kwamba Mugoya alikuwa akizuiliwa Kwa muda wa miaka mitatu, mahakama hiyo ilimfuga Kwa muda wa miaka 41.
Mnamo mwezi Septemba mwaka 2023, Mugoya alikiri kutekeleza mauaji hayo, ambapo alishtakiwa pamoja na washukiwa wengine saba.
Sheikh Mutumba aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 15 mwezi Januari mwaka 2020 katika wilaya ya Bugiri,muda mfupi baada ya kuongoza sala ya Ijumaa.
Mugoya ana siku 14 kukataa rufaa dhidi ya hukumu hiyo.