Urusi inavutiwa na madini ya Equatorial Guinea – Putin

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais Teodoro Obiang Nguema (kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia) mjini Moscow

Rais Vladimir Putin anasema kuwa makampuni ya Urusi yana nia “kubwa” katika kuchimba rasilimali za madini nchini Equatorial Guinea.

Amefanya mazungumzo na Rais wa Equatoguine Teodoro Obiang Nguema siku ya Alhamisi mjini Moscow, ambapo viongozi wote wawili walikubaliana kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

“Uwezo unaowezekana wa uwekezaji ni mkubwa, na uwezo wa nchi yako katika kuendeleza mahusiano haya pia ni mzuri,” Bw Putin alisema.

“Ninamaanisha kuhusu uwezo za zaidi unaohusiana na uchimbaji wa rasilimali za madini,” aliongeza.

Equatorial Guinea, nchi ndogo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa mafuta, imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi za madini kama vile dhahabu, almasi, urania na gesi.

Rais Nguema alisema amezikaribisha kampuni za Urusi zinazokuja kuwekeza nchini mwake.

Pia aliishukuru Urusi kwa kufungua tena ubalozi wake nchini Equatorial Guinea.

Share This Article