Waziri mkuu wa Ghana Mahamudu Bawumia amekubali kushindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumamosi huku akipongeza mwaniaji wa upinzani John Mahama kwa ushindi.
Mahama aliwahi kuhudumu kama Rais nchini Ghana na Bawumia amesema, “Watu walipigia kura mabadiliko”.
Uchaguzi huo umefanyika wakati ambapo taifa la Ghana linakumbwa na matatizo ya kiuchumi yaliyosababisha bei za bidhaa msingi kuongezeka mara dufu.
Ni wakati ambapo vijana pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira, na nchi imeshindwa kulipa madeni.
Tangazo la Bawumia la kukubali kushindwa hata hivyo linajiri wakati ambapo matokeo rasmi ya uchaguzi hayajatangazwa.
Tume ya uchaguzi ilitangaza kwamba matokeo rasmi yanahujumiwa na wafuasi wa vyama viwili vikuu nchini Ghana huku ikitaka maafisa wa usalama kuondoa wafuasi hao kwenye vituo vya kujumlisha kura.
Wafuasi wa Mahama tayari wamejitokeza kwenye barabara za maeneo mbali mbali ya Ghana kusherehekea ushindi wakiwa na imani kwamba atabadili hali.
Bawumia alisema alikubali kushindwa kutokana na hesabu za kura za chama tawala cha New Patriotic Party (NPP) ambazo zinaashiria kwamba Mahama ameshinda pakubwa.
Mahama kwa upande wake amekiri kwamba amewasiliana na Bawumia kwa njia ya simu na amempongeza kwa ushindi mkubwa.
Majibu hayo yasiyo rasmi yanadai kwamba ushindi wa Mahama ni wa kiwango cha asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa huku Bawumia akiwa na asilimia 41.
Lengo la Bawumia la kukubali ushinde mapema ni kuhakikisha mvutano unafikia kikomo na amani inasalia nchini Ghana.