Upigaji kura wa mapema unaendelea Zanzibar

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Uchaguzi wa mapema waendelea Zanzibar.

Zoezi la upigaji kura wa mapema linaendelea katika kisiwa cha Zanzibar leo Jumanne, kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Upigaji kura huo wa mapema, hutoa ruhusa kwa baadhi ya maafisa wa serikali  kupiga kura mapema, kwenye mpango ulioanzishwa kwa mara ya kwanza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Chama kikuu cha upinzaji, ACT Wazalendo, kinadai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hutumia mchakato huo kushawishi matokeo, kikidai CCM inatumia fursa hiyo kufanya ujanja kwenye uchaguzi.

Zanzibar ina historia ya uchaguzi unaokumbwa na msukosuko ambao miaka ya nyuma uligeuka kuwa mbaya na baadaye ukachochea kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kupunguza mvutano wa kisiasa.

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar yanatarajiwa kutangazwa ndani ya saa 24 baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika.

Website |  + posts
Share This Article