UoN yaimarika duniani

Boniface Musotsi
1 Min Read

Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) kimeimarika katika orodha ya vyuo vikuu duniani na pia bado kinashikilia uongozi nchini. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ambayo imetolewa, chuo hicho kimo kwenye mabano ya 900-950 ikilinganishwa na 1000-1200 ya mwaka jana.

Kwa mujibu wa tafiti hizo zilizofanywa na kituo cha kuorodhesha vyuo cha QS, kupanda ngazi huko kumetokana na kazi njema ya wafanyakazi na tathmini ya waajiri kuhusu ubora wa elimu wa chuo hicho.

Kutokana na wingi wa watafiti wa UoN ambao walifanya tafiti kutoka vitivo mbalimbali, walichangia pakubwa kuimarika huko kwani katika jukwaa la kimataifa, chuo hicho kilipata asilimia 50.1 ambayo ni ishara ya utajiri na utofauti wa ushirikiano katika utafiti.

Mwaka jana, UoN ilikuwa ya 1,425 kati ya vyuo 2,000 duniani. Barani Afrika, Chuo cha Cape Town-Afrika Kusini ndicho bora na kinaorodheshwa nambari 171 ulimwenguni. Chuo cha Teknolojia cha Massachusetts – Marekani, ndicho bora duniani.

Boniface Musotsi
+ posts
Share This Article