Umeme waanza kurejea Nigeria kufuatia giza totoro

Dismas Otuke
1 Min Read

Umeme umeanza kurejeshwa nchini Nigeria baada ya taifa zima kutumbukia katika giza totoro kufuatia kutoweka kwa umeme kwa zaidi ya saa kumi kutokana na moto uliozuka na kutatiza usambazaji umeme.

Umeme umekuwa ukipotea mara kwa mara nchini Nigeria na kisa cha hivi punde kuanzia mapema jana Alhamisi kiliathiri majimbo yote 36 na mji mkuu wa Abuja, kabla ya kurejeshwa katika maeneo kadhaa.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ameahidi kuimarisha usambazaji wa umeme kwa kuruhusu mashirika ya serikali kuunda mitambo yao ya kusambaza umeme.

TAGGED:
Share This Article