Ukaribu wa Juliet Zawedde na Chameleone wazua gumzo mitandaoni

Mfanyabiashara huyo alikatiza likizo yake nchini Uganda na kuandamana na Chameleone hadi Marekani kwa matibabu zaidi.

Marion Bosire
1 Min Read

Mfanyabiashara wa asili ya Uganda anayeishi Marekani Juliet Zawedde, amekuwa mtu wa karibu na wa msaada kwa mwanamuziki wa Uganda anayeugua Jose Chameleone.

Video ya wawili hao wakikaribia kupigana busu ilisambaa mitandaoni na kuzua gumzo, wengi wakishangaa iwapo wana uhusiano wa kimapenzi.

Zawedde alikuwa likizoni nchini Uganda Chameleone alipougua na kulazwa katika hospitali ya Nakasero na alimzuru hospitalini humo.

Baadaye binti huyo aliripotiwa kutoa mchango mkubwa uliofanikisha safari ya Chameleone hadi nchini Marekani kwa matibabu zaidi naye akakatiza likizo wakaandamana.

Anaripotiwa kuwa mwenyeji wa Chameleone kwa sasa huko Boston, Massachusetts nchini Marekani pamoja na kakake Weasel Manizo.

Ripoti za awali zinaashiria kwamba wamekuwa marafiki wa muda mrefu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *