Ujumbe wa kwanza wa Kenya kwa mashindano ya Riadha Ulimwenguni kuondoka Jumatatu usiku

Dismas Otuke
1 Min Read

Ujumbe wa kwanza wa timu ya Kenya itakayoshiriki mashindano ya Riadha Ulimwenguni utaondoka nchini Jumatatu usiku kuelekea Budapest Hungary, kwa makala ya 19 yatakayoandaliwa kuanzia Jumamosi hii hadi Agoisti 27.

Ujumbe huo wa kwanza unawajumuisha wanariadha na maafisa 19 kwa jumla na utafuatwa na ujumbe wa pili utakaondoka nchini Jumanne utakaowajumuisha  wanariadha na maafisa 39 kwa jumla .

Ujumbe wa tatu utaabiri ndege Alhamisi ukiwa na wanariadah na maafisa jumla ya 16 na kisha ujumbe wa mwisho utakaowashirikisa wanariadha wa mbio za marathon ukitarajiwa kuondoka  Agsoti 22 na utawajumuisha wanariadha 10.

Kenya italenga kuboresha matokeo ya mwaka uliopita mjini Oregon Marekani ilikozoa dhahabu 2 ,fedha 5 na shaba 3.

Wanariadha Emmanuel Korir na Faith Kipyegon ndio pekee watakotea mataji yao mwaka huu.

Kikosi cha Kenya kinawajumuisha wanariadha 57 .

Mashindano hayo yatarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.

 

Website |  + posts
Share This Article