Ujenzi wa uwanja wa Talanta Sports City kugharimu bilioni 44.7

Waziri Tuya amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo umefikia asimia 37, na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2026.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa ujenzi wa uwanja wa Talanta Sports City, utagharimu shilingi bilioni 44.7.

Akizungumza alipofika mbele ya Kamati ya Bunge inayosimamia Michezo, Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya, alisema tayari kampuni ya ujenzi kutoka China imelipwa shilingi bilioni 2.

Tuya, aliongeza kuwa ujenzi wa uwanja huo umefikia asimia 37 na unatarajiwa kukamilika Februari 28, 2026.

Aidha, Waziri alisema kuwa shilingi zingine bilioni 3.6 zinatumika kwa awamu ya kwanza ya ukarabati wa uwanja wa Kasarani na kiwango kingine cha bilioni 3.1 ili kuuwezesha uwanja huo kuandaa kipute cha CHAN mwezi Agosti mwaka huu.

Shilingi zingine bilioni 1.1 zitagharimia ukarabati unaoendelea wa uwanja wa Nyayo, wakati ukarabati wa nyuga za Police Sacco na Ulinzi Complex ukiigharimu serikali shilingi milioni 582 na milioni 490 mtawalia.

Website |  + posts
Share This Article