Waziri wa Madini Hassan Joho na Gavana wa Kwale Fatuma Achani wamezindua ujenzi wa soko la kisasa la samaki eneo la Mwaepe, wadi ya Kinondo, katika kaunti ndogo ya Msambweni.
Mardi huo wa gharama ya shilingi bilioni 256 unaofadhiliwa na benki ya dunia na umeasisiwa na shirika la Kemfsed kupitia kwa serikali ya kaunti ya Kwale, unalenga kuimarisha biashara ya vijana wa sekta ya Jua Kali na wavuvi.
Mradi huo wa mamilioni ya pesa utashuhudia ujenzi wa soko la kisasa la samaki wa barafu, karakana, maegesho ya boti, afisi za usimamizi wa ufukwe, jumba la mikutano, mikahawa miwili, na vibanda vya kuuza bidhaa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Joho ameutaka utawala wa kaunti ya Kwale chini ya uongozi wa Gavana Achani, kukabiliana na unyakuzi wa ardhi ya umma kwa kurejesha ardhi iliyonyakuliwa.