Ujenzi wa kanisa Ikulu wasitishwa na Mahakama Kuu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama Kuu imesitisha ujenzi wa kanisa latika ikulu ya Nairobi na Rais William Ruto, kusubiri uamuzi wa kesi mwezi Novemba.

Mahaka imesema serikali isitishe ujenzi wowote wa kanisa katika Ikulu ya Nairobi au Ikulu yoyote ndogo nchini hadi kesi iliyowasilishwa kupinga ujenzi huo itakapoamuliwa.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Chacha Mwita amesema ujenzi wa kanisa katika Ikulu na ikulu ndogo hauruhusiwi hadi kesi zilizowasilishwa zitakapoamuliwa Novemba 18 mwaka huu.

Rais Ruto alikuwa ameanzisha ujenzi wa kanisa la shilingi  takriban bilioni 1.2 mwezi uliopita.

Share This Article