Klabu ya General Service Unit (GSU) ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Voliboli (KVF) kwa wanaume msimu wa mwaka 2024 na 2025, baada ya kuwachabanga Kenya Ports Authority (KPA), seti tatu kwa bila katika mechi ya tatu ya fainali Jumapili alasiri katika ukumbi wa Karasani.
GSU wamesajili ushindi wa seti tatu bila za 25-19, 25-21 na 25-22.
Ilibidi timu hizo zicheze mechi ya tatu leo baada ya GSU kushinda siku ya Ijumaa nao KPA wakaibuka washindi jana.
GSU wameshinda taji ya kwanza ya ligi kuu tangu mwaka 2022 na ya 16 jumla huku wakifuzu kushiriki mashindano ya Afrika msimu ujao.
Equity Bank walichukua nafasi ya tatu huku Kenya Prisons wakiridhia nafasi ya nne.