Rwanda imesitisha uanachama wake katika Jumuia ya uchumi wa mataifa ya Afrika ya kati (ECCAS).
Rwanda ilitangaza kujiondoa siku ya Jumamosi kwa kile ilichokiatja kuwa udikteta wa uongozi baada ya ECCAS, kwenda kinyume na maafikiano ya kongamano la Malaba, lilipendekezwa Urais wa Jumuia hiyo kuzunguzwa miongoni mwa mataifa wanachama.
Aidha, Rwanda imesema imetamaushwa na hatua ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) kuendelea na kuhimiza utawala wa kimabavu katika jumuia hiyo.
Yamkini uhasama kati ya Rwanda na DRC umechangia kujiondoa kwa Rwanda baada ya DRC kukataa kuhudhuria kongamano lilikuwa liandaliwe Rwanda na kubidi kuhamishwa.
Mataifa hayo yamekuwa na mzozo kuhusu vita vya kundi la waasi wa M23 mashariki mwa Congo ambao yamkini wanafadhiliwa na serikali ya Rwanda .
ECCAS inajumuisha mataifa 11 wanachama, ambayo ni Angola, Burundi, Cameroon, Afrika ya Kati , Congo, Gabon, Equatorial Guinea, DRC, Rwanda , Sao Tome Principe na Chad.