Ujenzi wa barabara za lami Kwale kufaidi wakazi

KBC Digital
1 Min Read
Ujenzi unaoendelea wa barabara za lami katika kaunti ya Kwale

Katika juhudi za kuimarisha miundombinu ya barabara katika kaunti ya Kwale, serikali ya kaunti hiyo imeendeleza ujenzi wa barabara za lami katika kaunti hiyo.

Barabara za hivi punde kuwekwa lami ni barabara ya Kona Polisi hadi hospitali kuu ya rufaa ya Msambweni pamoja na ile ya Tiwi – Vinuni, barabara ambazo zinatarajiwa kusaidia wakazi katika maeneo hayo na uchukuzi hasa kwa wanaotafuta huduma za serikali ikiwemo katika hospital kuu ya rufaa ya Msambweni.

Hadi kufikia sasa, serikali ya kaunti ya Kwale kwa kipindi cha miaka miwili, imekamilisha ujenzi wa kilomita 20.za barabara za lami ndani ya kaunti hiyo ikiwemo barabara ya Mwangwei-Majoreni, huku ujenzi wa barabara ya lami ya kutoka Tiwi hadi Vinuni ukijumuisha kilomita 10.8 za barabara zinazoendelea kutengenezwa.

Wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Najma Mohammed, wametaka kuharakishwa kwa ukarabati wa barabara hizo wakisema kwa muda mrefu wagonjwa pamoja na kina mama waliotaka kujifungua walipitia changamoto zaidi kutokana na hali mbaya ya barabara.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *