Uingereza wahemeshwa na Nigeria kabla ya kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Uingereza almaarufu Three Lionesses wamekabiliwa na wakati mgumu dhidi ya Nigeri Superr Falcons kabla ya kuwashinda kupitia matuta ya penalti na kujikatia tiketi kwa robo fainali ya Kombe la Dunia kwa akina dada mjini Brisbane nchini Australia.

Timu hizo zilitoka sare tasa baada ya dakika 90 kabla ya Uingereza ambao ni mabingwa wa Ulaya kushinda penalti 4 -2 na kutinga hatua ya nane bora.

Lauren James alipigwa kadi nyekundu kwa kumkanyaga mchezaji  wa Nigeria Michelle Alozzie mwishoni mwa mechi.

Uingereza watachuana na mshindi kati ya Jamaica na Colombia katika hatua ya kwota fainali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *