Uhuru ahudhuria misa ya wafu inayoandaliwa na upinzani

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amehudhuria misa ya wafu inayoandaliwa na muungano wa upinzani Azimio la Umoja One Kenya, mtaani Karen kuwakumbuka Wakenya wanaodaiwa kuangamizwa na polisi wakati wa maandamano wiki iliyopita. 

Uhuru aliwasili katika eneo la SKM Centre tayari kwa maombi akijiendesha kwa gari lake.

Ni kikao cha kwanza kwa Uhuru kukutana hadharani na viongozi wa upinzani tangu akabidhi mamlaka kwa Rais William Ruto.

Wandani wa Ruto wamekuwa wakimshutumu rais huyo wa zamani kwa kufadhili maandamano ya kupinga serikali yaliyoitishwa na muungano wa Azimio.

Uhuru amekanusha madai hayo.

Hata hivyo, hatua yake ya kuhudhuria ibada hiyo huenda ikaibua ukosoaji mkubwa kutoka kwa viongozi wa utawala wa Kenya Kwanza wanaohisi anahujumu utendakazi wa serikali baada ya jitihada zake za kumuunga mkono Raila katika uchaguzi mkuu uliopita kuambulia patupu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *