Uhispania wamefuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda Uswidi mabao 2-1 katika nusu fainali iliyochezwa leo Jumanne uwanjani Eden Park nchini Australia.
Salma Paralluelo alipachika bao la ufunguzi kwa Uhispania kunako dakika ya 81, kabla ya Uswidi kujibu kupitia kwa Rebecka Blomqvist dakika ya 88.
Sherehe za Waswidi zilizimwa ghafla bin vuu baada ya beki Olga Carmona Garcia kuwarejesha Uhispani uongozini kwa goli la dakika ya 89 na kuwapa ushindi wa kihistoria.
Uhispania watakutana na mshindi wa nusu fainali ya pili ya Jumatano baina ya Uingereza na wenyeji wenza Australia kwenye fainali ya siku ya Jumapili.
Uswidi watachuana na mshinde kati ya Australia na Uingereza kuwania nishani ya shaba.