Uhispania wameikwatua Uingereza mabao 3-0, mapema leo na kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 .
Nusu fainali hiyo ya pili ilisakatwa katika uwanja Olimpico Felix Sanchez, katika Jamhuri ya Dominica.
Alba Cerrato na Paula Commenaddor walifunga bao moja kila mmoja, huku Zara Shaw, akijifunga kwa Uingereza na kuwapa Wasponyola ushindi huo.
Uhispania watamenyana na Korea Kaskazini katika fainali ya Jumapili baada ya Korea kuishinda Marekani bao moja kwa sifuri katika nusu fainali ya kwanza.
Marekani na Uingereza zitachuana Jumamosi kuwania nishani ya shaba.