Uhispania, Scotland na Uturuki wafuzu kwa fainali za Euro 2024

Dismas Otuke
1 Min Read

Uhispania ukipenda La Roja, Scotland na Uturuki zilijikatia tiketi kwa kipute cha fainali za kombe la Euro mwaka ujao nchini Ujerumani, baada ya mechi za jana Jumapili usiku.

Uhispania wakicheza ugenini walisajili ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Norway katika kundi A, Gavi akipachika goli la pekee.

Uhispania wakisherehekea bao la ushindi dhidi ya Norway

Georgia iliwanyuka Cyprus mabao manne kwa ombwe katika pambano jingine la kundi A.
Ushindi wa Uhispania uliwafuzisha Scotaland, timu zote zikiwa na alama 15 baada ya mechi sita.

Uturuki waliichakatua Latvia magoli manne kwa sifuri wakiwa nyumbani Istanbul na kufuzu wakiongoza kundi D kwa pointi 16.

Uturuki wakisherehekea kufuzu kwa dimba Euro mwaka 2024

Croatia waliambulia kichapo cha 2-1 ugenini mjini Cardiff dhidi ya Wales katika mkwangurano mwingine wa kundi hilo.

Mataifa 7 yamewahi tiketi za kindumbwendumbwe cha kuanzia Juni mwaka ujao wakiwemo wenyeji Ujerumani, Uhispania, Uturuki, Scotand, Ubelgiji, Ufaransa na Ureno.

Share This Article