Uhispania wamenyakua kombe la dunia kwa wanawake kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda Uingereza bao moja kwa bila kwenye fainali ya kusisimua iliyosakatwa Jumapili katika uwanja wa Olimpic Mjini Sydney Australia.
Olga Carmona alipachika bao la pekee na la ushindi kwa Uhispania maarufu kama La Roja.
Jenifer Hermoso alipoteza penati ya kipindi cha pili .
Uhispania sasa imenyakua kombe la dunia kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 na wale wasiozidi umri wa miaka 20.