Uhispania na Ureno zitamenyana kwenye awamu ya 16 bora ya Kombe la Dunia baada ya kushinda mechi za raundi ya 32 Alhamisi usiku.
Uhispania iliwakomoa Austria mabao 3-0, Mikel Oryazabal akifunga mawili naye Pedro Porro akaongeza jingine katika mechi ya Alhamisi usiku uwanjani Los Angeles, Marekani.
Katika pambano la mapema Ijumaa, Ureno walifuzu baada ya kuwazidia maarifa Croatia magoli 2-1 kiwarani Toronto, Canada.
Croatia walitangulia kufunga kupitia kwa Ivan Perisic dakika ya 53 kabla ya nahodha Cristiano Ronaldo kusawazisha dakika ya 68 kupitia penalti, kisha Goncalo Ramos akapachika goli la ushindi kunako dakika ya 94.
Uhispania na Ureno watakaoandaa makala ya mwaka 2030 ya Kombe la Dunia watakabiliana Julai 6 mjini Dallas, kuwania tiketi ya robo fainali.