Uhamishaji wa majukumu yaliyogatuliwa, wadau wakutana

Martin Mwanje
1 Min Read

Kamati ya kiufundi ya uhusiano baina ya serikali, IGRTC leo Jumatano asubuhi ilishiriki mkutano wa ushauriano na taasisi za serikali na Baraza la Magavana, CoG kuhusiana na ukamilishaji wa uhamishaji wa majukumu yaliyogatuliwa. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na makatibu wakuu wakiongozwa na Teresia Mbaika wa ugatuzi, timu ya IGRTC ikiongozwa na mwenyekiti wake Kithinji Kiragu, Afisa Mkuu Mtendaji wa CoG Mary Mwiti na maafisa wa kiufundi kutoka taasisi mbalimbali za serikali.

Washikadau walipitia upya kazi iliyofanywa na timu 12 za sekta mbalimbali na kuangazia masuala yanayoibuka.

Aidha walitoa mchango wao kuhusiana na mikutano ya ngazi za juu iliyopangwa kufanywa wiki ijayo kwa mujibu wa agizo la mkutano wa 10 wa viongozi wakuu la kumaliza zoezi hilo la uhamishaji majukumu ndani ya siku 60.

IGRTC inatarajiwa kuchapisha notisi za gazeti rasmi la serikali, ripoti za sekta mbalimbali na mipango ya utekelezaji ili kuchochea uhamishaji wa rasilimali husika.

 

Website |  + posts
Share This Article