Ugonjwa usiojulikana wawaua watu zaidi ya 50 DRC

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Ugonjwa usiojulikana wawauza watu zaidi ya 50 DRC.

Ugonjwa usiojulikana ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa watoto watatu waliokula popo, umesababisha vifo vya watu zaidi ya 50 kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC. Shirika la SAfya Duniani WHO, limethibitisha hayo.

Mkurugenzi wa Matibabu wa Hospitali ya Bikoro, ambayo ni kituo cha ufuatiliaji cha kikanda alisema muda kati ya kugunduliwa kwa dalili hadi kifo, umebainishwa kuwa saa 48 katika visa vingi.

Mlipuko wa hivi punde wa ugonjwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulianza Januari 21, na visa 419 hadi sasa vimenakiliwa huku vifo 53 vikiripotiwa.

Kulingana na afisi ya Afrika ya shirika la afya duniani-WHO, mlipuko wa kwanza katika mji wa Boloko ulianza baada ya watoto watatu kula popo na kufariki ndani ya saa 48 kufuatia dalili za homa ya kuvuja damu.

Baada ya mlipuko wa pili katika mji wa Bomate mnamo Februari 9, sampuli kutoka kwa kesi 13 zilitumwa kwa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba ya Kibiolojia katika mji mkuu wa Kongo, Kinshasa, kwa uchunguzi.

Sampuli zote hazikuwa na ugonjwa wa  Ebola au magonjwa mengine ya kawaida ya kutoka damu kama Marburg. Wengine walipimwa na kupatikana kuwa na malaria.

Website |  + posts
Share This Article