Uganda kuwaondoa wanajeshi Mashariki mwa DRC

Wizara ya Ulinzi ya Uganda, imesema usalama wa mji huo utakabidhiwa kwa jeshi la DRC (FARDC).

Tom Mathinji
1 Min Read
Uganda kuwaondoa wanajeshi Mashariki mwa DRC.

Jeshi la Uganda (UPDF) limetangaza kuondoka katika mji wa Lubero, Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), katika muda wa wiki mbili zijazo.

Wizara ya Ulinzi ya Uganda, imesema usalama wa mji huo utakabidhiwa kwa jeshi la DRC (FARDC) baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Uganda.

Vikosi vya Uganda vimekuwa vikiendesha operesheni tangu Januari 2025, kupambana na kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF).

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Kanali Chris Magezi, Kaimu Mkurugenzi wa Habari katika jeshi la UPDF, haikufafanua sababu za uamuzi wa kuwaondoa wanajeshi hao kutoka Lubero.

Hatua hii inajiri wakati kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, uliosababisha DRC kuitisha ubalozi wa Uganda kufuatia taarifa za mtandaoni zilizotolewa na Mkuu wa Majeshi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

TAGGED:
Share This Article