Ufaransa yatakiwa kusitisha ubaguzi wa rangi

Tom Mathinji
1 Min Read

Siku kadhaa baada ya polisi nchini Ufaransa kumpiga risasi mvulana wa umri wa miaka 17, Umoja wa Mataifa umeitaka Ufaransa kushughulikia masuala ya ubaguzi wa rangi.

Polisi nchini Ufaransa walimpiga risasi na kumuua Nahel M, katika kizuizi cha polisi cha barabarani, siku tatu zilizopita na kusababisha maandamano makubwa nchini humo.

Katika juhudi za kutuliza hali nchini humo, Rais Emmanuel Macron aliongoza mkutano wa dharura kuhusu ghasia zilizoikumba Ufaransa tangu wakati huo, na kuacha msururu wa majengo yanayoteketea, magari yanayofuka moshi na kuporwa kwa majengo ya umma.

Serikali ya Ufaransa inasema inafanya kila iwezalo kurejesha utulivu.

Miji mitatu mikubwa nchini humo – Paris, Marseille na Lyon – inasimamisha au kuzuia usafiri wa umma kuanzia Ijumaa jioni.

Takriban watu 900 wamekamatwa huku maafisa 250 wa polisi wakijeruhiwa.

Machafuko pia yameshuhudiwa katika eneo la Bahari ya Hindi la Ufaransa la Réunion.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *