Ufaransa yaondoa majeshi yake Niger

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa nchi yake itaondoa majeshi na balozi wake kutoka nchini Niger kufuatia mapinduzi ya Rais Mohamed Bazoum mwezi Julai mwaka huu.

Wanajeshi 1,500 wa Ufaransa ambao wamekuwa nchini Niger wanatarajiwa kuondolewa ifikiapo mwishoni mwa mwaka huu.

Tayari Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS imeiwekea vikwazo Niger kufuatia mapinduzi hayo.

Mataifa ya eneo la Sahel ambayo ni Niger, Mali na Burkina Faso yamekumbwa na mapinduzi ya serikali.

Share This Article