Ufanisi wa CHAN wamwongezea Muchiri cheo jeshini

Muchiri aliye n umri wa miaka 26 amepandishwa mamlaka kutoka Senior Private  hadi Corporal.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wingá wa Harambee Stars Boniface Muchiri amepandishwa cheo katika jeshi la Kenya, kufuatia ufanisi wake kwenye michuano ya kombe la CHAN mwaka huu.

Muchiri aliye n umri wa miaka 26 amepandishwa mamlaka kutoka Senior Private  hadi Corporal.

Halfa hiyo ya kupandishwa cheo kwa Muchiri iliandaliwa jana na Mkuu wa Majeshi Charles Kahariri.

Nahodha huyo wa klabu ya Ulinzi Stars amekuwa nguzo muhimu kwa Harambee Stars akiiongoza kucheza hadi robo fainali ya kipute cha CHAN kwa mara ya kwanza, akichangia mabao mawili dhidi ya Madagascar na dhidi ya Zambia.

Website |  + posts
Share This Article