Uenyekiti wa AUC: Ruto, Uhuru wampigia debe Raila

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta wametoa wito kwa Wakenya na washikadau wa kimataifa kuuunga mkono juhudi za Raila Odinga kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC. 

Wawili hao wametoa wito huo wakati Ruto alipomtembelea Uhuru nyumbani kwake huko Gatundu leo Jumatatu.

“Viongozi hao wawili walitoa wito kwa Wakenya, marafiki wa Kenya, na washikadau wa kimataifa kuunga mkono ugombea wa Raila Odinga kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika,” ilisema taarifa kutoka kwa msemaji wa Ikulu ya Nairobi Hussein Mohamed.

Raila amekuwa akitembelea mataifa mbalimbali ya bara la Afrika kutafuta uungwaji mkono wakati uchaguzi wa kumteua mwenyekiti mpya wa AUC ukiwa umepangwa kufanywa mwezi Februari mwakani.

Mwenyekiti anayeondoka wa AUC ni Moussa Faki Mhamat kutoka Chad.

Raila anasemekana kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *