Ligi mpya ijulikanayo kama UEFA Super League, itabuniwa ilivyokuwa awali baada ya mahakama ya muungano wa mataifa ya Ulaya kusema Alhamisi kuwa shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA na Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, hawakuwa na haki ya kusimamisha ligi hiyo iliyokuwa ianze mwaka 2021.
Uamuzi huo unaruhusu kuanza kwa upya kwa ligi hiyo iliyoasisiwa na kinara wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez,na ilikuwa inajumuisha timu 20 za wanaume zikiwemo 12 ambazo ni waanzilishi.
Timu kuu barani Ulaya zilizosaini kujiunga na ligi hiyo ni 6 za kutoka Uingereza zikiwemo Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham, Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid kutoka Uhispania na vilabu vya Italia AC Milan, Inter Milan na Juventus.
Wadadisi wanahisi ligi hiyo itakinzana na ligi ya mabingwa barani ulaya ambayo ni mashindano makubwa zaidi baina ya vilabu .