UDA na ODM wabuni muungano wa kisiasa kuelekea 2027

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Rais William Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) na Orange Democratic Movement (ODM), chake Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga vimebuni muungano wa ushirikiano kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Hafla ya kusaini muungano huo imeandaliwa leo Ijumaa katika ukumbi wa Jumba la Mikutano ya Kimataifa, KICC.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wabunge na viongozi wakuu serikalini.

Wafuasi wa vyama vyote viwili walijiung na viongozi wao Ruto na Raila kushuhudia hafla hiyo.

Akihutubu wakati wa uzinduzi huo, Raila amesema aliafikia uamuzi huo baada ya kushauriana na wafuasi wake katika maeneo mbalimbali humu nchini.

Raila amesema kuwa baadhi ya mapendekezo yake ni kuhakikisha mgao wa pesa za kaunti unaongezeka hadi shilingi bilioni 450.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *