Chama cha United Democratic Alliance, UDA kitafanya uchaguzi wake mwezi Disemba mwaka huu kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Haya yametangazwa Jumamosi na Rais William Ruto akiwa eneo la King’ong’o kaunti ya Nyeri alipofungua afisi ya chama cha UDA.
Ruto anayezuru kaunti ya Nyeri amesema wanalenga kuwachagua viongozi watakaoimarisha chama kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Hata hivyo, hatima ya chama cha Ford Kenya kinachoongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula na ANC chake kinara wa mawaziri Musalia Mudavadi haijulikani na ikiwa watalazimishwa kuvunja vyama vyao.