Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.5

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali inalenga kutekeleza mikakati itakayo hakikisha uchumi wa taifa hili unakua kwa asilimia 5.5 katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025.

Hayo yalisemwa Leo Alhamisi na Waziri wa fedha Prof. Njunguna Ndung’u, alipowasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/2025 katika majego ya bunge.

Kulingana na Prof. Ndung’u, mikakati hiyo ni pamoja na kuwekeza pakubwa katika maendeleo ya nguvukazi, ustawi, ulinzi na udhibiti wa soko, utumizi wa rasilimali za hapa nchini, mageuzi katika taasisi za serikali na utekelezaji wa dijitali katika usimamizi na ufufuzi wa uchumi.

Waziri huyo alidokeza kuwa ili kuafikia ukuaji huo, serikali pia itafanya mabadiliko katika sekta ya kilimo, itawasaidia wanabiashara wadogowadogo na kufanikisha ukuaji wa kidijitali.

Aidha  Prof. Ndung’u alisema serikali itapiga jeki sekta ya ubunifu ili kusaidia kubuni nafasi zaidi za ajira.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *