Uchumi wa Kenya umeimarika, Baraza la Mawaziri laarifiwa

Tom Mathinji
2 Min Read
Rais William Ruto,aongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri.

Rais William Ruto leo Alhamisi aliongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya Nairobi.

Katika mkutano huo, Baraza hilo lilifahamishwa kuwa uchumi wa taifa ni thabiti, huku mfumko wa bei ukipungua hadi asilimia 2.7 mwezi uliopita kutoka asilimia 9.6 mwezi Septemba mwaka 2022.

Kulingana na mkutano huo, kiwango hicho ndicho cha chini zaidi tangu mwaka 2007, wakati wa hatamu ya Rais Mwai Kibaki.

Kadhalika, bei ya bidhaa za vyakula imepungua hasaa mahindi, maharagwe  na mbaazi, imepungua katika muda wa miaka kadhaa.

Kuhusu ubadilishanaji wa sarafu za kigeni, mkutano huo ulifahamishwa kuwa shilingi ya Kenya inadizi kuimarika huku ikishuka hadi 129 kutoka 162.

Kwa upande wa mapato ushuru uliokusanywa na halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini uliongezeka kwa asilimia 11.5 kufikia mwezi Juni mwaka huu.

Baraza hilo liliarifiwa kwamba hali ya chakula nchini ni thabiti kutokana na mpango wa serikali ya kupunguza bei ya mbolea miongoni mwa hatua nyingine.

Baraza hilo pia lilijadili na kuidhinisha sera kadhaa ikiwemo kupandishwa hadhi kwa taasisi tano za mafunzo ya kiufundi kuwa vyuo vya kitaifa vya mafunzo anuwai.

Hiv ni pamoja na vile vya Michuki, Mitunguu, Nairobi na chuo cha utafiti na teknolojia cha Friends huko Kaimosi.

Vyuo vya kitaifa vya mafunzo anuwai sasa vitaongezeka kutoka 23 hadi 28.

Na kuhusiana na utekelezaji wa halmashauri ya afya ya kijamii baraza hilo liliarifiwa kwamba wafanyakazi wa zamani wa NHIF watahamishiwa kwenye idara nyingine serikalini na kwamba hakuna yeyote atakayepoteza ajira.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article