Uchaguzi wa makamishna wa AUC kukamilika leo Ethiopia

Dismas Otuke
1 Min Read

Uchaguzi wa makamishna wa tume ya Umoja wa Afrika (AUC) ulioanza jana katika kikao cha 46 mjini Addis Ababa, Ethiopia, unatarajiwa kukamilika leo.

Uchaguzi huo unawashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na utafuatiwa na ule wa Marais, watakaopiga kura kati ya Jumamosi na Jumapili hii kumchagua mwenyekiti mpya wa AUC.

Kiti hicho kinawaniwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, Waziri wa Mambo ya Nje ya Djibouti, Mahamoud Ali Youssouf na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Madagascar, James Richard Randamandriato.

Washindi wa viti vya makamishna, mwenyekiti na naibu ni sharti wapate theluthi mbili ya kura zote za mataifa wanachama yanayoruhusiwa kupiga kura.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *