Waasi M23 watishia kutwaa mji wa Bukavu

Dismas Otuke
1 Min Read

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda wameapa kutwaa mji wa Bukavu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

M23 wamesema kuwa hali inazidi kudorora na watapanua utawala wao hadi Bukavu baada ya serikali ya Rais Felix Tshisekedi kukataa kuwashirikisha katika mazungumzo ya kuleta amani.

Endapo M23 watatwaa Kivu Kusini, huenda mapigano mapya yakazuka katika mpaka wa Burundi na DRC, kati ya M23 na wanajeshi wa Burundi wanaounga serikali ya Tshisekedi.

M23 walitisha mapigano baada ya kongamano la pamoja kati ya Jumuia ya Afrika Mashariki EAC na Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuamrisha kusitishwa kwa mapigano ili kuruhusu mazungumzo ya mani yaliyokuwa yashirikishe kila upande.

Chama tawala cha Tshisekedi cha UPDS kilitangaza juzi kuwa watazungumza tu na M23 iwapo makundi mengine yatashirikishwa pia.

.

Website |  + posts
Share This Article